CORRECT LYRICS

Lyrics : Nenda Lote

Ohh, na, na, na, na, na

Umetuma wazazi wako waje wanielezee
Umetuma wazazi wako waje wanielezee
Hunitaki tena, na mashoga zako waje waniambie
Na mashoga zako waje waniambie
Ndoa tumeivunja

Siamini kuna time singeishi bila wewe
Mapenzi ya kukata na shoka, eh, eh
Yashamwagika, hayazoleki haya, oh
Basi nenda lote, mama
Nenda lote, mama

Mpenzi, unaenda
Nilikuenzi kinomanoma
Yashamwagika, hayazoleki haya, oh
Nenda lote, mama

Ukatuma lawyer wako aje anisomee
Ukatuma lawyer wako aje anisomee
Kuwa watoto ulionizalia, eh, eh
Kuwa watoto ulionizalia, eh, eh
Sitawaona tena
Uhh

Siamini kuna time tuliapa hadharani
Kanisani kwa chanda na pete, eh
Yashamwagika, hayazoleki haya, oh
Nenda lote, mama
Nenda lote, mama

Mpenzi, unaenda
Nilikuenzi kinomanoma
Yashamwagika, hayazoleki haya, oh
Nenda lote, mama

Ukatuma pastor wako aje anikemee
Ukatuma pastor wako aje anikemee, mama
Na madeni zangu ukazitangaza, eh (Ukazitangaza, eh)
Na madeni zangu ukazitangaza, eh
Mitandaoni, oh
(Mitandaoni, oh, eh)

Shemeji zangu, ndugu zako, tukionana
Waambie sisi bado rafiki, eh, eh
Wasinipite barabarani, mama, oh
Umeenda lote, mama
Umeenda lote, mama

Mpenzi, unaenda (Mpenzi, oh, baby)
Nilikuenzi kinomanoma (Oh, jana, no, no)
Yashamwagika, hayazoleki haya, oh
Basi nenda lote, mama
Nenda lote, mama
Mpenzi, unaenda (Mpenzi, eh)
Nilikuenzi kinomanoma (Eh, yeh, yeh, yeh, yeh, yeh, yeh)
Yashamwagika, hayazoleki haya, oh (Hayazoleki haya, oh)
Nenda lote, mama (Mama, mama)
Nenda lote, mama