CORRECTAR LA LETRA

Letra : AYA

Mmmmh mmmmhh

[Verse One]
Ndo kusema kwamba
Nina bahati mbaya ama nyota imefifiaa
Maana sio kweli kila siku mimi ndo naumiaaa
Ndo kusema kwamba sura yangu mbaya
Haina hulka ya kuvutia
Maana sio kweli kila siku mimi ndo naumiaaa

Ina maana penzi lingekua chombo cha usafiri
Ningekosa hata sehemu ya kusimama
Ningewezaje nitawezaje
Au labda mapenzi hufaa kwa matajiri
Halafu mi apa sina maana
Sa nitaanzaje nitaanzaje

Inawezekanaje nikose kufurahi
Siku zote ninazoishi na uhai
Najua mungu hapendi walimwengu mna via
Nikisema niage nitakua najilaghai
Moyo utakuwa bado unanidai
Acha niweke imani ipo siku nitaridhishwa

AYA, AYA, AYA, AYA

[Verse Two]
Na sinacho maanisha mnakijua
Kuyakosa mapenzi inanitesa
Sawa nakua nayaona
Sa mbona yananizidia
Hivi ninacho maanisha mnakijua
Upweke  unanitesa

Halafu nakua nayaona
Wengine wana enjoy aaah
Ingekuwa gambe ndo dawa ya mawazo
Ningekunywa nilewe aah
Nilewe nilewe nilewe

Inawezekanaje nikose kufurahi
Siku zote ninazoishi na uhai
Najua mungu hapendi walimwengu mna via
Nikisema niage nitakua najilaghai
Moyo utakuwa bado unanidai
Acha niweke imani ipo siku nitaridhishwa

AYA, AYA, AYA, AYA