CORRECT LYRICS

Lyrics : Sitaki

Mimi wewe mimi ntakufa na wewe
Mimi wewe mimi ntakufa na wewe

Ni baraka za mungu na malaika
Zimefanya mi nawe tujuane
Sinashaka maana imeandikwa
Ndege warukao wafanane
Sisikii la muadhini wala la mnadi swala
Tumelishana ya mini kwa dua sio kafara
Sio wanyuzi tisini wala buku shing'dala
Mambo ya kuzini zini tuwe halali twahara

Kama mapenzi ugonjwa wa macho mi kabisa kengeza
Na kama changuoni ndo kikulacho mi huyu kanimeza

Na sitaki nishauriwe, sitaki nishauriwe
Na sitaki nishauriwe, sitaki nishauriwe

Ngamia wangu anifaae jangwani
Nimemuombea dua tusiishie njiani
Ngamia wangu anifaae jangwani
Nimemuombea dua tusiishie njiani
Ooh usingizi wangu zeze la kitandani
Nimemuombea dua tusiishie njiani
Ngamia wangu anifaae jangwani
Nimemuombea dua tusiishie njiani

Kama mapenzi ugonjwa wa macho mi kabisa kengeza
Na kama changuoni ndo kikulacho mi kwangu kanimeza

Na sitaki nishauriwe, sitaki nishauriwe
Na sitaki nishauriwe, sitaki nishauriwe

Aiih makopa kanimwagia makopa jama
Aiih makopa kanimwagia makopa jama
Ma ma ma ma kanimwagia makopa jama
Aiih makopa kanimwagia makopa jama
Mwa mwa mwa kanimwagia makopa jama
Aiih makopa kanimwagia makopa jama