CORRECT LYRICS

Lyrics : Ndoto Ya Mchana

Niliskia tufununu, Kwamba ulipata mwingine,
Anayekupenda zaidi ya mimi, mtafunga ndoa
pengine,
Yetu ilikuwa shadow, mapenzi yenu yamekolea,
Lazima huwa Anakupa, vitu sikuwa nakupea,
Ndoto zako zote, ulizoniambia,
Naona kama kweli sasa zinatimia,
Na Sina chochote, cha kukuambia,
Ila nakonda Kweli nikikufikiria,

Hook
Sura yako umbo lako jamani eeh,
Busu na mahaba chumbani maami ,
Mawaidha yako nikiwa matatani eeh,
Nikikumbuka najiona hayawani maami

Chorus:
Nawatakia mema, (Nawatakia mema)
Nawatakia mema, (Nawatakia mema)
Nawatakia mema, (Nawatakia mema)
Basi kwaheri kwaheri kwaheri Mami (Ndoto
yangu ya Mchana)

Ingawa inaniuma, niko na furaha moyoni,
Kuona kwamba umepata, vyote ulivyokuwa
unatamani,
Naomba nipate mwaliko, wa harusi nije Nile

wali,
Nipige picha na wadau, nikupe zawadi kama
zamani
Alafu ntapeform, kama beshte yako, kale
kawimbo nilikuimbia shambani
Na nitakuinform, tunza mume wako, Japo kuna
vitu zenye ninatamani,

Hook:

Chorus
Ingawa ningependa,ungekuwa wangu pekee,
(Nawatakia mema)
Ingawa moyoni umeniachia kidonda, (Nawatakia
mema)
Namwomba Mungu, anipatie mwingine Kama
wewe, (Nawatakia mema)
Hivo kwaheri kwaheri kwaheri kwaheri mama
(Ndoto yangu ya Mchana)
Lakini ninaomba, unifanyie favour Moja
(Nawatakia mema)
Ukijifungua kama ni wa kiume,mpe jina laangu
(Nawatakia mema)
Na kama ni wa kike mpe jina la mama yangu
(Nawatakia mema)
Basi kwaheriiiiiiii (Ndoto yangu ya Mchana)