CORRECT LYRICS

Lyrics : Corona

Ee Mola
Waja wako tumesimama, tuonyeshe suluhisho
Kutwa tumeshika tama, Hatuishi masikitiko
Ama hizi ndo zile zama, ziloandikwa za mwisho
Mtoto analia baba mama, wote manung'uniko

Nilidhani utani, wanatudanganya
Waongo nikawaona, nikawaona
Si unajua vijana wa maskani, wajuaji sana
Eti, Bongo hakuna Corona, Corona

Mara kitimu timu
Nasikia habari, kila nikipita
Waziri Umi mwalimu
Katangaza tayari, kuna waadhirika
Makundi kundi matimu
Tamko la serekali, marufuku kukusanyika
Ukanipata wazimu
Nitapata wapi ugali? Show zote zimevunjika

Mmmh sekondari, primary, na vyuo vyote vifungwe
Ukiona una mbaya dalili, muone doctor usivunge
Eeh hili ngojwa hatari, kabisa tujichunge
Usije ukafanya siri, itakuua

Corona, corona eeh! Unataka nini?
Corona, corona eeh! Kwetu umefuata nini?
Corona, corona eeh! Umekosea nini?
Corona, corona eeh! Utaondoka lini?

Moyo umetanda hofu, masikini mimi
Ndugu zangu walotoka Europe, wote wako karantini
Ishamkumba SK, wasi wangu Salam
Na yule Mwana FA, washaposti Instagram
(Sorry, naomba kurudia kidogo kipande hiki kimenihuzunisha sana)
Ishamkumba SK, wasi wangu Salam
Na yule Mwana FA, washaposti Instagram
Eeh na sasa Wasafi kweupe, hakuna watu ofisini
Naona marupe rupe, jamani tuwe makini

Sekondari, primary, na vyuo vyote vifungwe
Ukiona una mbaya dalili, muone doctor usiunge
Eeh hili ngojwa hatari, kabisa tujichunge
Usije ukafanya siri, itakuua

Corona, corona eeh! Unataka nini?
Corona, corona eeh! Kwetu umefuata nini?
Corona, corona eeh! Umekosea nini?
Corona, corona eeh! Utaondoka lini?

Mikono kwa sabuni, osha osha
Kwa sekunde ishirini, osha osha
Vaa mask usilete uhuni, osha osha
Ukiwa nyumbani ofisini, osha osha