CORRECT LYRICS

Lyrics : Wandoto

Yeah, oh na wo wo
Yeah yeah woo

Nahisi kama naota
Na kumbe reality tayari
Aliyefanya nateseka, ni wewe
Na nafsi inachochota
Najipa imani sijafeli
Nahitaji faraja hata chembe nipewe maa
Macho pembeni nisikupe pesa
Kwako yaani nishafika
Kumbe makucha uliyaficha na ushanikwarua ooh
Na zangu hisia umeziteka
Nilipokosea sawazisha
Usije hadharani kuanika ukaniumbua
Oh nah nah nah

Na nakuombea Mungu
Akuepushe na mabaya
Hali dhiki mafungu
Ila la kwangu ndo limepwaya
Nalia nalia kwa uchungu
Umenitoroka nyuma ya idhaya
Ni wewe japo nilikudhamini na nikakuitaga

Wandoto wandoto
Wandoto, wandoto
Ah ni wewe wa ndoto
Leo penzi umeliweka vikwanzo
Wandoto wandoto
Wandoto, wandoto

Wandoto uliyekuwa ni wewe
Na kichwa umekiachia mawazo
Oooh ooh, aah yeah yeah
Kweli usiku wa giza usilolijua
Sikuwaza, sikudhania kuwa utanibagua
Sa unafikiri nani wa kupika pakua, ni wewe
Kishida kijiba cha roho mwenzako naugua
Haya no commando siwezi jipindua
Nawe ndo dereva umezamisha mashua
Ni wewe ni we eh
Ila mwenzako bado bado
Moyo unasonona
Manati bila kipago
Nikuulize wapi uliona
Mi nina uzoefu wa kufunga goal
Uvivu wa kufua foronya
Yaani siamini yes umegeuza no
Na kwako mi mtoto nahitaji nyonya

Wandoto wandoto
Wandoto, wandoto
Ah ni wewe wa ndoto
Leo penzi umeliweka vikwanzo
Wandoto wandoto
Wandoto, wandoto