CORRIGER LES PAROLES

Paroles : Nani

Hmm yeah
Hmmmmm yeah

Asubuhi kumekucha
Wingu limetanda
Na mvua yata kunyesha
Na uko mbali mama
Maji takitiririka
Oh baridi itanishika
We ndo chanda chema uhakika unanikatisha tamaa                
Utaambiwa binadamu
Ah kila mmoja ana mapungufu yake
Sijui nilipoteleza mama, si ungeniambia
Nimemiss tabasamu, kutwa kucha picha kummezea mate
Yangu fimbo umeibeza, ah katu hautaki kuitumia
Labda hesabu za kutoa mi niligawanya baby unisamehe
Na ile hasi nikafanya chanya baby unisamehe
Na hata emoji za kulia nazo kutumia nazo zikome
Japo nipate furaha, ah huruma unionee

Maana hii hali, hata haifichiki
Kutwa wima cha mpingo, kisiki
Maana hata nikiona michezo ya njiwa
Ah huwa naitamani kama si wewe

Nitampenda nani
Nitampenda nani
Nitampenda nani
Nani nitampenda
Nitampenda nani
Nitampenda nani
Nitampenda nani
Nani nitampenda aah

Eh penzi usifanye kwa chombo cha usafiri
Ikawa umeshuka uje utanikatili
Nitakuwaga mental Niko dhahari, si unasikia
Penzi la dhati daima la wawili
We fanya na urudi lisiwe batili
Ka wafanya kusudi ni ukatili mi naumia

We ndo yangu hifadhi labda nilikosea msimbo
Kweli kupenda kazi wangu umegeuka fimbo o
Mi ndo lako koroboi
Lile lisilo zima
Aha si ulisemaga hauchomoi
Kumbe imani ulinipima ah
Pia ulisema haudonoi
Wameiteka mazima
Ahaa simung unyi sikohoi
Sina vyangu nimechina

Maana hii hali, hata haifichiki
Kutwa wima cha mpingo, kisiki
Maana hata nikiona michezo ya njiwa
Ah huwa naitamani kama si wewe

Nitampenda nani
Nitampenda nani
Nitampenda nani
Nani nitampenda
Nitampenda nani
Nitampenda nani
Nitampenda nani
Nani nitampenda ah