CORRECT LYRICS

Lyrics : Bachela

Eti Lava utaoa lini, mbona unazingua?
Wazuri wengi mjini, wezi wanachukua
We kutwa ubishoo, nywele kuchange mitindo
Wanakuona wafoo, kila siku uko single

Moyo wa kupenda sina ya nini nijipe homa
Si huyu ni mwana Stamina rafiki yake Roma

Si unajua, ndoa majaliwa nasubiria apange Maulana
Atanitunukia, bado naula ujana

Ujana maji ya moto utakuunguza (Nitakuunguza)
We pita peku mpoto tutakuuguza

Kwanza kuolewa raha, oh nah nah wili wili
Ona mume wangu hii spa, atumiliki wawili wili

Umenikumbusha kule Insta udaku
Wanasema mume umekwara
Ati umefuata hela, ukakubali kuolewa mitara

Hutanishauri mimi, wakati wangu ndo sasa
Mimi mtoto wa mjini
Kula bila shida chini, acha nile bata
Nijipe stress za nini?

Bora niwe bachela
Sitaki kujifunga funga, kujibana bana
Niwe bachela
Kwanza naona mapenzi Faida hayana

Bora niwe bachela eh
Huo ni utoto unajidanganya
Niwe bachela
Unayoyafanya mwisho hayana
Bora niwe bachela!

Dada Darleen acha kunichachafya
Uliza kilomkuta Dangote
Sijui kangombana na Tanasha
Ametu-unfollow wote

Mapenzi ya siku hizi
Shemeji Lokole mwongoza umbea
Mkigombana tu kashatizi Insta nzima yameshaenea

Ndio maana nimetulia
Navuta pumzi staki kwenda mbio
Mambo ya kujifanya hodari eti mjuzi
Ujuzi huo kwio

Tukiachana na yote
Mimi bado sikuungi mkono
Wasafi wote
Mnaonekana mnapenda ngono

Hutanishauri mimi, wakati wangu ndo sasa
Mimi mtoto wa mjini
Kula bila shida chini, acha nile bata
Nijipe stress za nini?

Bora niwe bachela
Sitaki kujifunga funga, kujibana bana
Niwe bachela, kwanza naona mapenzi
Faida hayana

Bora niwe bachela eh
Huo ni utoto unajidanganya
Niwe bachela
Unayoyafanya mwisho hayana

Mabachela piga kelele(Weee)
Piga kelele moja(Weee)
Kelele mbili(Weee weee)
Piga kelele tatu(Weee...)

Wenye wapenzi piga kelele(Weee)
Walio oa(Weee)
Tulio olewa je?(Weee...)